TMDA YATAHADHARISHA WANANCHI KUACHA KUNUNUA BIDHAA AMBAZO HAZIJASAJILIWA NA KUTHIBITISHWA.
Na.Vero Ignatus,Arusha
Mamlaka ya Vifaa Tiba TMDA Kanda ya kaskazini imetoa wito kwa jamii kuwa makini wakati wanaponunua dawa na kuwataka kuzichunguza vizuri kabla ya kuzitumia na kama watakuwa na mashaka juu ya dawa hizo, watoe taarifa kwa Mamlaka hiyo ili hatua za haraka za kisheria zichukuliwe
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kaskazini TMDA Proches Patrick kwenye Maonyesho ya sikukuu za nanenane viwanja vya Themi Jijini Arusha 8/8/2022,kwamba dawa bandia ni tatizo kwani wapo waingizaji na wasambazaji ambao siyo waaminifu ,wanaojali maslahi yao kuliko Afya za walaji, jambo ambalo husababisha madhara kwa binadamu,na kupunguza uaminifu kwenye mfumo mzima wa utoaji huduma ya Afya.
Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kaskazini TMDA aliainisha baadhi ya dawa zilizokamatwa na Mamlaka hiyo,ambazo hazijasajiliwa ni Pamoja na 60 minutes- Male Genital Desensinsitizer Spray (The Delay Spray for men) inayosababisha kuchelewa kufika kileleni kwa mwanaume,Pamoja na Increase MK II Men’s Penis enlargement) kuongeza maumbile kwa wanaume
‘’Dawa hizi tumezikamata hazijasajiliwa na wala hazina vibali vya usambazaji na uuzaji wa dawa hizo nchini,na wala sisi kama TMDA hatujaitathimini na kusajili dawa hizi kabla ya kuruhusiwa kuingia sokoni maana sisis tunasimamia ubora usalama na ufanisi wa dawa vifaa tiba na vitendanishi .Alisema Proches
Adha alisema kuwa lengo kuu la Mamlaka hiyo kushiriki katika maonyesho ya sikukuu ya nanenane ni kutoa elimu kwa wananchi kwani Aya yao ndiyo mtaji wao hivyo wakiwa na afya bora wataweza kufanya shughuli za uzalishaji mali,na uchumi vizuri.
TMDA imewataka Wananchi kutambua kuwa kutumia bidhaa ambazo hazijasajiliwa ni kuhatarisha Afya zao,maana hawajui mtengenezaji alikuwa anakusudia kutengeneza kitu gani ,hivyo jukumu kubwa ni kuhakisha kwamba vitu ambacho mwananchi wanakitumia ni kile ambacho Mamlaka imethibitisha.
‘’Mamlaka inaendelea kuwakamata wale wote wanaovunja sheria na kuwafikisha mahali panapowastahili, wananchi nunueni bidhaa kwenye maduka yaliyosajiliwa na TMDA na Tasisi za Serikali ,msinunue kwenye vyombo vya usafiri,wala wale wanaopitisha bidhaa mkononi ,nunueni sehemu ambayo mtapewa risiti halali’’Alisisitiza
Aidha maonyesho hayo ya 28 ya Nanenane 2022 yamebeba Kauli Mbiu isemayo Ajenda 10/30 Kilimo ni Biashara Shiriki Kuhesabuiwa kwa Mipango Bora ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi.
Mwisho.
No comments