RC MONGELLA :ASILIMIA 3% YA PATO LA TAIFA HUPOTEA KWA KUSHUGHULIKIA MASWALA AMBAYO YANALETWA NA UNYANYASAJI WA KIJINSIA
Ilikomesha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ni muhimu kuwawezesha wanawake ili kujikwamua kiuchumi na kijamii,kwani asilimia 3% ya pato la taifa hupotea kwasababu ya kushughulikia masuala ambayo yanaletwa na unyanyasaji wa kijinsia
Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani 8machi 2022 mkoani Arusha, katika uwanja wa kumbukumbu wa shekh Ameri Abeid kwamba ukatili utakapokomeshwa itasaidia kuokoa rasilimali fedha nyingi zinazopotezwa kutokana na athari za unyanyasaji na kutokuwa na usawa wa kijinsia.
‘’Mimi naamini wanaume wenzangu sasahivi tunajihisia Amani na rah asana kuliko tunavyodhaniwa maana yake kuna wakati wanadhani wanaume tunawasiwasi sasahivi ndio tuna amani nafuraha kubwa zaidi kwasababu tuanajua jamii yetu ilivyo,wakina mama hawa wakienda mbele wakawa na nguvu zaidi hata sisi maendeleo hayo yatatugusa
Naibu Waziri wa Katiba na sheria Mhe.Geofrey Pinda Amesema kuwa kamati hizo zikisimamiwa kama inavyotakiwa itapunguza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwani umiliki wa ardhi umekuwa ni kizungumkuti kwa wakinamama kwani hawapewi nafasi saw ana baba hivyo wizara inaendelea kuliangalia sualahilo
Pinda amesema kuwa Maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani ninkutathimini na kuheshimu mchango wa mwanamke duniani katika nyanja zote za uchumi kiutamaduni,kisiasa kijamii katika kuleta Maendeleo katikabya kweli ukizingatia kuwa katika tamaduni.
Pinda amesema kuwa katika mizunguko ambayo amekuwa nikiiifanya kuzungukia mikoa kuwasikiliza wananchi matatizo ya wananchi mengi kati yao yamekuwa suala la ndoa,mirathi na migogoro ya ardhi hivyo serikali inaendelea kulifanyia kazi katika kulichakata.
Kwa upande wake Naibu katibu mkuu wa wa wizara ya maendeleo ya jamii jinsia ,wanawake na watu wenye mahitaji maalum Amon mpanju ameiomba mikoa kuhakikisha kuwa inaanzisha na kusimamia kamati za ulinzi wa wanawake na watoto yaani MTAKUWA ili jamii jamii iweze kushiriki katika kupambana na vitendo vya ukatili nchini .
No comments