RC MONGELA: USAWA WA KIJINSIA SIYO KWA WANAWAKE PEKEE BALI KWA KILA MTU AMBAYE MAISHA YAKE YATABADILIKA KUTOKANA NA DUNIA YENYE USAWA.

Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela akiwa na Afisa Maendeleo ya jamii mkoa wa Arusha Blandina Nkini,wakitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya maandalizi ya siku ya wanawake duniani machi 8

Na.Vero Ignatus,Arusha 
 
Katika kuelekea kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka machi 8 siku hiyo hutolewa  wito wa kuhakikisha uwezeshaji na usawa wa Kijinsia

Akizungumza na vyombo vya habari  Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela amesema kuwa, Faida za usawa wa kijinsia sio tu kwa wanawake na wasichana bali ni kwa kila mtu ambaye maisha yake yatabadilika kutokana na dunia yenye usawa.
 
 Mongela amesema kuwa tarehe nne wanawake watatembelea wodi za kinamama katika hospitali ya Levolosi  na kufanya usafi kutoa misaada ya vifaa katika wodi za kinamama,hivyo ni vyema watanzania wengine wakaungana nao katika shughuli hiyo yenye tija katika jamii.

 Amesisitiza kuwa  amesema kuwa usawa wa kijinsia unapaswa kupewa kipaumbele na ushiriki wa wanawake katika maadhimisho hayo yatakayoenda sambamba na matukio kadhaa hadi kilele.

Ameitaja  Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ya wiki ya siku ya wanawake duniani "Haki usawa kwa maendeleo endelevu tujitikeze kuhesabiwa"

Pia alibainisha kwamba tarehe 5 wanawake watapata fursa ya kutembelea hifadhi ya Ngorongoro na Mgeni Rasmi atakuwa Mary Masanja Naibu waziri Maliasili na Utalii sanajari na mbio za kilometa tano na kumi kwa wanawake

Kwa Upande wake Afisa Maendeleo ya jamii mkoa wa Arusha Blandina Nkini alifafanua kuwa mbio hizo mgeni Rasmi atakuwa Pauline Gekul sanjari na Kongamano la wanawake litakaloendeshwa na chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru.

Bi Nkini amefafanua  zaidi shughuli za siku hiyo kwamba siku ya tarehe 7 kutakuwa na maonesho ya watoa huduma za wanawake itakayoenda sambamba na siku ya kilele uzinduzi wa kanzi data ya wanawake na uongozi Tanzania 

Aitha amebaisnisha kuwa  Mgeni rasmi wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani atakuwa Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi Maalumu Doroth Gwajima.
 
 Ikumbukwe kuwa Siku hiyo ilianza kuadhimishwa tarehe 8 Machi 1975 baada ya Umoja wa Mataifa kuridhia siku hii kutumika  kama siku rasmi ya kuikumbusha dunia juu ya haki za wanawake.
 
Siku hii pia huongeza chachu katika harakati za mapambano katika usawa wa kijinsia kwa wanawake na wanaume katika jamii. Aidha maadhimisho ya siku hiyo kwa mwaka huu yamebeba ujumbe wa usawa kwa watu wote.

Siku ya wanawake duniani kwa mara wa kwanza ilisherehekewa katika mwaka wa 1911 ambapo mataifa 11 yalikusanya wanawake mia moja walipoanza kuadhimisha siku hii ambapo Mwaka 1908 jumla ya wanawake 15,000 waliandamana katika katika mji wa New York  wakidai kupunguziwa muda wa kufanya kazi ,kupata ujira wa kuridhisha na kupewa haki ya kupiga kura

Mwaka 1909 mwanamke kwa jina la Clara Zetkni alipendekeza kuanzishwa kwa siku ya wanawake duniani katika mkutano wa wafanyakazi wanawake uliofanyika katika jiji la copenhagen nchini Dermark 

 

Mwisho

 
 

No comments