WAALIMU:TUJENGEWE UWEZO JUU YA MTAZAMO MPYA WA ELIMU
Na Vero
Ignatus,Arusha
Waalimu wameomba kujengewa uwezo kupitia semina
mbalimbali ili kuwasaidia kupata mbinu mbalimbali za kujenga mwanafunzi umahiri
pamoja na kuwajengea uelewa na ubunifu
Akizungumza
mwalimu wa taaluma Mary Shayo
kutoka shule ya msingi Elikiurei:Ni kwamba waaalimu wajengewe uwezotangia
mtaala mpya ulioletwa waalimu hawajawahi kuwezeshwa lakini kupitia warsha kama hii
waalimu tutapata uwezo wa kuwaelekeza wanafunzi h
Dkt.Fika
Mwakabungu ni
Mkurugenzi wa mafunzo na Mitaala kutoka taasisi ya taasisi ya Elimu Tanzania ,katika kongamano
lililoandaliwa na Taasisi ya The
foundation for tomorrow juu yamtazamo mpya wa elimu,kwamba waalimu wanatakiwa
kujiongeza katika ufundishaji wa kupambanua vitu
‘’Tunatakiwa
kujiongeza kwelikweli katika ufundishaji wetu tupambanue vitu tunjenga watu wa kujiajiri au wa kuajiriwa
sasawatoto nao wanakuwa wakali kweli kweli,tuweke vitu ambavyo watavikiri
,watavichambua na kuona viko sawa’’alisema Mwakabungu
Dkt.Mwakabungu alisema kuwa Taasisi ya elimu
Tanzania hivi karibuni imekuwa ikikusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wa
elimu kuhusiana na mitaala iliyopo katika elimu ambayo waalimu wanaitekeleza.
‘’Wathibiti
ubora wanakwenda kuangalia je mitaala hii inakwenda kumjenga huyu mtoto ambae
tunamtaka ? tulifanya uwasilishaji mkubwa dar es salaam dodoma na Zanzibar,kilichoonekana
ni kwamba mitaala nimizuri mno lakini tatizo lipo kwenye utekelezaji ,kwani ni
kwa namna gani kunawawezesha waalimu ili waweze nao kuwekeza kwa wanafunzi’’alisema
Mwakambungu
Alisema kuwa
ni vyema waalimu wakajiuliza ni namna
gani wanawafundisha wanafunzi, katika kutengeneza
au kukuza ujuzi kwa waalimu ,mafunzo katika mikakati bora ya ufundishaji
wasasa,kuanzisha ukosoaji , thamini pamoja na ufundishaji unaomzingatia mwanafunzi
na kuleta ubunifu badala ya kukariri.
Kwa upande wake Mratibu wa mafunzo kwa waalimu
kutoka taasisi ya Foundation for tomorrow Adrean Maganga alisema kuwa
lengo la mafunzo hayo ni kuongeza /kukuza ujuzi kwa waalimu,kutengeneza
muungano wa/mtandao wa waalimu Tanzania,uboreshaji wa morali,kwa utambuzi wa
kazi ya ualimu na kuridhika kwao kutasababisha hamu ya kujifunza zaidi
,kuipenda kazi yao,hatimae kuelekea muungano wa na ustawi wa kada ya ualimu
katika jamii.
Maganga
alisema kuwa mafunzo hayo katika mkakati wa wa ufundishaji wa sasa,kuanzisha
ukosoaji wa thamani endelevu,tafakuri na kuanzisha michakato ya uboreshaji,utasababisha
ufundishaji unaomzingatia mwanafunzi na kuleta ubunifu katika ufundishaji.
‘’Waalimu
ambao wanahisi kushikamana hujisikia kuwa na ujasiri na kuthaminiwa jambo
ambalo linahimiza waalimu kupata taarifa na rasilimali zaidi na kuongeza tabia
ya kushirikiana ‘’alisema Maganga
Malengo ya taasisi hiyo kukuza ujuzi wa waalimu,ikiwa ni pamoja na mafunzo katika mikakati bora ya ufundishaji wa sasa,kuanzisha ukosoaji na thamani endeleu ,tafakari,na kuanzisha michakato ya uboreshaji,ambayo itasababisha ufundishaji unaomzingatia mwanafunzi na kuleta ubunifu katika ufundishaji.
Kutengeneza muungano au mtandao wa waalimu nchini Tanzania,kwasababu waalimu wanaposhikaman hujisikia kuwa na ujasiri,na kuthaminiwa ,hii ni sambamba na uboreshaji wa morali kwa waalimu
MWISHO
No comments