ICT TUPIENI MACHO SUALA LA UKATILI WA KIJINSIA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII KWA WANAWAKE

Mkutano wa Mwaka 5 waTEHAMA  unaendelea katika Kituo Cha Kimataifa Cha Mikutano AICC Jijini Arusha
Mulembwa Munaku Mkurugenzi wa Tehama Wizara ya  Habari  ,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari akizungumza na waandishi wa habari kwenye Mkutano wa Mwaka unaendelea Jijini Arusha
Neema Lugangira Mbunge wa viti Maalum CCM ambaye anawakilisha Asasi za Kiraia NGO kutoka Tanzania Bara akizungumza anwandishi wa habari katika Mkutano wa tano Mwaka unaendelea Jijini Arusha
Wadau wa Mkutano wa Mwaka 5 wa TEHAMA wakiwa katika Kituo Cha Kimataifa Cha Mikutano AICC Jijini Arusha

ICT  TUPIENI MACHO SUALA LA UKATILI WA KIJINSIA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII KWA WANAWAKE 

Na.Vero Ignatus,Arusha.

Mkutano wa tano Mwaka wa TEHAMA unaendelea Jijini Arusha ,ukiwa na lengo la kuwaunganisha wadau wote wa tehama,kutoka sekta za Umma na Binafsi ili kujadiliana Maendeleo ya Tehama Nchini

Neema Lugangira  Mbunge wa viti Maalum (CCM) ambaye anawakilisha Asasi za Kiraia NGO kutoka Tanzania Bara,  amesema  kwamba  suala la kunufaika katika tehama ni pamoja na Ushirikishwaji wa makundi yote wakiwemo wanawake ,kwani kumekuwa na ukuaji mkubwa wa ukatili wa Kijinsia kwenye mitandao ya kijamii 

Tunapoongelea ukuaji wa  kidigitali lazima tuangazie Usalama kwenye mitandao ya kijamii kwa makundi yote ikiwemo kundi la wanawake kwenye siasa.Alisema Rugangira(Mb) 

Lugangira amesema kuwa Jambo hilo limekuwa  kisababishi ambacho  vinapelekea wanawake kuogopa kuingia kwenye siasa,maana wanajua wakiingia hawatakinzana kwa hoja bali  watu kwenye mitandao  watajibi,ana nao kutokana na uanawake wa mtu husika

Mimi nikiwa Kama mwanamke kwenye siasa (mb)nimejaribu kuwaeleza wadau wa ICT  iko haja ya kuangalia Ukatili wa Kijinsia unaowekwa kwenye wanawake walioko kwenye siasa,kwani ni kati ya  ,hivyo inapelekea ushiriki wawanawake kwenye siasa ,unakuwa mdogo,pia inapelekea wale wanaotamani kuingia kwenye siasa wanahofu ya kuingia kwenye siasa.Alisema Rugangira 

Sambamba na hayo ametoa pendekezo kwa ICT Kuona  nchi inakuwa na   Sera za  uchumi kidigitali ,Sera mkakati na mfumo ambao utapelekea ukuaji wa sekta ya Tehema 

Tukikinfanisha na wenzetu wa Kenya wanazonsera hizi zote,na wao kwenye taarifa zao rasmi unasema kwamba hii sekta ya digitali inachangia kwa 8%kwenye Pato ghafi,lakini pia inatengeneza ajira zaidi ya 250,000,vilevile ndio sekta inayokua kwa Kasi" Alisema Neema

Akizungumza na waandishi wa habari  MKURUGENZI wa TEHAMA Mulembwa Munaku ,kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya habari ambae pia ni mwenyekiti wa Kongamano hilo,amesema kuwa kwa Sasa hivi yapo mabadiliko makubwa ya tehema nchini na mtu anaweza kutumia simu yake ya mkononi na  akafanya biashara ya mtandaoni

Munaku ametoa wito kwa  Wazazi wote na Jamii kwa ujumla ,waweze kuhakikisha kwamba, vijana wanatumia tehama kwa mtumizi sahihi ili iwasaidie katika makuzi yao,kwa kutafuta fursa mbalimbali za kipato na kiuchumi

Akijibu swali aliloulijwa juu ya ukuaji wa Tehama na athari kwa vijana :Changamoto kubwa haswa ipo kwa vijana 75% hivyo Kama wanahitaji kujenga Taifa sahihi  lenye mahitaji ya tehama ,lazima tujikite Kama Serikali tuwekeze tuangalie ni namna gani tutawasaidia vijana

Munaku alisema kutokana na changamoto hizo wamejipanga na kuwaunganisha wadau na kuanza  kupeleka na kuongeza Elimu kwa vijana ,kwa matumizi ya tehama, pia wananchi wanapaswa kufahamu kuwa siyo jukumu la Serikali pekee, bali kila mdau anawajibika kuanzi ngazi ya shuleni,familia kuhakikisha kijana aliyenae nyumbani aweze kukutumia katika njia iliyo sahihi.

Alisisitiza kuwa Matarajio ya wananchi ni kupata elimu, ambayo kama Taifa lilivyopiga hatua katika masuala ya Tehama, mtandao,pia watarajie  kuangalia namna watakavyopata wawekezaji  katika tehama,na mazimio ambayo watayapata kwenye kikao hicho ,watayafanyia kazi ili waweze kupiga hatua kwa kuwasaidia wananchi na kuongeza ajira

Aidha mkutano huo wa siku tatu unaendeleaje Jijini Arusha katika Kituo Cha Kimataifa Cha AICC,umehudhuriwa na wadau  zaidi ya wadau 600 ,wengi wao wamejiunga kufuatilia kwa kupitia njia ya mtandao,ambapo utafunguliwa na kufungwa hapo siku ya ijumaa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa 

Mwisho







No comments