Baraza la Habari Tanzania (MCT) Lasikitishwa na wanahabari waoga
Kajubi Mwakajanga Katibu mtendaji Baraza la habari Tanzania. Picha na Vero Ignatus
Msemaji katika mkutano cr huo Owino Opondo kutoka nchi ya Kenya.Deus Kibamba kutoka Taasisi ya kijamii ya Umoja, Haki ya kupatq Taarifa akiongoza katika uchokonozi wa majadiliano. Picha na Vero Igna
Salim Salimu Msahauri na Mtaalamu wa maswala ya Habari (mwandishi mkongwe mstaafu) akichangia mada katika mkutano mkuu wa Mwaka Baraza la Habari Tanzania. Picha na Vero Ignatus
Mkuu wa Chuo cha Practical School of Journalism (PST) Kiondo Mshana akichangia mada
Baadhi ya washiriki wakiwa katika mkutano wa wa mwaka ulioandaliwa na Baraza la habari Tanzania (MCT) uliofanyika katika hoteli ya Ocean View Zanzibar.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa Baraza la Habari Tanzania wakiwa katika mkutano kwenye ukumbi wa Zanzibar Ocean View.
Mkutano ukiendelea. Picha na Vero Ignatus
Na Vero Ignatus, Zanzibar
Waandishi wa habari kutoka maeneo tofauti Nchini wameonyesha kuchukizwa na vitendo vya kuminywa uhuru wa kutoa na kupokea habari jambo ambalo wamesema ni kinyume na katiba
Wakichangia katika mkutano maalumu juu ya ufinywaji wa mashirikiano ya jamii na Vyombo vya habari ulioandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) ambao ulifanyika Zanzibar, wamesema vitisho vimekuwa vikubwa na ufungiaji vyombo onyo.
Mtaalam na mshauri wa habari nchini Salim Said Salim amesema wanachokifanya watawala ni kuwatisha wandishi ili wasifichuliwe maovu yao na kuweleza waandishi wakati huu ni muhimu sana kwao na wasiogope wafanyekazi zao kwa kufuata maadili ya kazi zao.
“licha ya uwepo wa hali hii ambayo ni ngumu kwetu hatupaswi kuogopa badala yake tutekeleze kazi zetu kwa mujibu wa maelekezo ya fani yetu maneno ya wakubwa tuayapinga” alieleza Salim.
Alisema kuwa kuwepo kwa vikwanzo hivyo wazione kama ni changamoto ambazo wanaweza kuzieepuka kwani Tanzania ni ya watu wote si ya mtu mmoja.
“yaani tifanyeni kazi mpaka ifike wakati Serikali na taasisi zote zile ziheshimu waandishi wa habari na kazi zao” alieleza.
Akitolea ufafanuzi kuhusu changamoto hizo katibu mtendaji wa baraza la habari Tanzania Kajubi Mukajanga alisema ni kweli kuna changamoto kubwa hivi sasa ya vitisho lakini alifahamisha njia pekee ya kukabiliana na vitisho hivyo ni waandishi wote Tanzania kuwa umoja wenye nguvu.
Aliwataka waandishi hao wakisikia miongoni mwao amepatwa na kadhia hizo basi kila mmoja aone imemfika yeye na kuaza kutafutanjia ya kulitatua kwa ppamoja.
“Lakini havi vitimbi vyao havitakuwa na nafasi kama tutakuwa tunaandika habari ambazo ni za kweli na zenye kufuata maadili” alieleza Kajubi.
Akizungumza katika mkumbi huo mkufunzi wa mkutano huo Owino Opondo alieleza kuwa licha ya kufungiwa vyiombo lakini ni jambo la kusikitisha kupigwa ovyo kwa wanahabari hapa nchini.
“Leo limekuwa jambo kawaida kumuona mwaandishi anapigwa na vyombo vya dola na bila hofu , tunahitaji umoja ulio na nguvu ya kweli” alieleza Opondo.
James Marenga ambaye Mjumbe wa Taasi ya Umoja wa kupata habari Tanzania ambaye ni mwanasheria aliwataka waandishi wa habari kutowa mashirikiano wakati wakati wanafikwa na matatizo mbali mbali.
“Unaweza kumuona mwaandishi anapata matatizo lakini inapofika wakati wa kutoa ushahidi anakimbia kabisaa, jambo ambalo na sisi kama watetezi linatuvunja moyo” alieleza Marenga.
Waandishi wa habari zaidi 200 Tanzania wamekutana katika mkutano siku moja Zanzibar ili kuona njia gani wataweza kufanya utetezi na kuondoa ule ufinyu wa ushirikiano jamii na vyombo vya habari.
No comments