ARUSHA UNITED YAJIGAMBA KUWAPIGA VIBONDE WA KUNDI GREEN WARRIORS

 Wachezaji wa Arusha United ‘wanautalii’ wakiwa katika mazoezi katika Uwanja wa Maj . Gen. Isamhuyo Mbweni Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wao wa leo jioni dhidi ya Green Warriors FC
Kocha mkuu wa Arusha United ‘WanaUtalii’ Fred Felix Minziro akitoa maelekezo kwa wachezaji wa Arusha United.


Na. Vero Ignatus

 Timu ya Arusha United Sports Club ‘WanaUtalii’ inajitupa leo uwanjani kupambana na timu ya Green Warriors ya Dar es Salaam katika mchezo wa kutafuta pointi tatu katika ligi la Daraja la Kwanza.  

Kocha mkuu wa Arusha United Fred Felix Minziro amesema kikosi kipo imara na hakuna majeruhi yoyote hivyo wanategemea kuibuka na ushindi utakaoifanya timu iendelee kukaa kileleni. 

Mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa leo majira ya saa kumi jioni katika viwanja vya Maj. Gen. Isamhuyo Mbweni Dar es Salaam. 

Arusha United inaingia dimbani ikiwa na rekodi ya kushinda mechi mbili na kutoa droo mechi moja.

No comments