ACHENI IMANI POTOFU JUU YA WANAWAKE MIGODINI,WAPENI NAFASI NI WAAMINIFU , WANAWEZA.

Mwenyekiti wa Kamati ya Madini ya Vito Femata Nchini Prosper Daudi Tesha , ambaye  Mkurugenzi wa Kampuni ya R-Gi investimet . 

Afisa madini mkazi Arusha Bertha Luzabuka:wanawake wengi wanamwamko wa kufanya kazi mbalimbali za kujiingizia kipato bila kujali ugumu wa kazi huku wengine wakikabiliwa na majukumu ya kuendesha familia zao. 

Wanawake wa jamii ya Kimaasai wanaojipatia kipato Chao kwa kutafuta kwenye udongo unaotolewa katika mgodi wakiwa katika picha ya pamoja na RMO katika eneo la Mundarara wilayani Long I do Mkoa wa Arusha

Katika picha ni baadhi ya wakinamama qa jamii ya Kimaasai wa kwanza kushoto ni Ngidai Mollel :Tumeweza kujenga nyumba zetu, kusomesha watoto kwa kuokota vipande vidogovidogo vinavyosalia kwenye udongo unaotoka mgodini. 

"Wanawake ni waaminifu wakipata kipato chao kinakwenda Mojave kwa moja kwenye familia":Tesha

Na. Vero Ignatus Arusha. 

ACHENI IMANI POTOFU JUU YA WANAWAKE MIGODINI,WAPENI NAFASI NI WAAMINIFU , WANAWEZA. 

KATIKA Kulelekea  kilele cha sherehe za siku ya wanawake Diniani ambayo kitaifa itafanyika Jijini Arusha Marchi  nane, Waajiri wa sekta ya madini wametakiwa kuwapa kipaumbele wanawake katika ajira kutokana  na kundi hilo kuwa waaminifu katika utendaji wa kazi

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Madini ya Vito Femata Nchini Prosper Daudi  Tesha wakati akiongea na Waandishi wa habari na kuongeza kuwa Serikali kwa sasa ina budi kuwaamini Wanawake katika fursa mbalimbali aambazo zinajitokeza ikiwemo sekta madini.

‘’Wanawake wakipewa nafasi za kufanya kazi wanaweza kwani kwa sasa wamekuwa wakifanya kazi katika maeneo mbalimbali huku waajiri wao wakionyesha kuwaamini hata katika vitengo vikubwa  vilivyopo katika maofisi  hapa nchini’’.

Tesha ambaye pia ni Mkurugenzi wa  wa Kampuni ya R-Gi investimet alisema kuwa Wanawake kwa kuaminiwa wamekuwa wakifanya vizuri hali ambayo hata wakipata fedha zimekuwa zikienda kwa kiasi kikubwa katika kulea familiaaaa.

Aidha Mwenyekiti huyo aliendelea kusema kuwa katika migodi sasa hata wanawake wamekuwa ni wamiliki na wawekezaji wakubwa katika skta ya madni huku akitolea mfano wa Kuwepo kwa chama cha wachimbaji Madini cha Wanawake Nchini (TAWOMA) ambacho kwa sasa kimekuwa kikimliki migodi mikubwa.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa Femata alisema kuwa wao katika shughuli za kiuchimbaji wanapenda kuwa pamoja na wanawake hali ambayo hata kazi zao zinakuwa zikifanyika bila ya kuwa na wasiwasi wa aina yeyote..

Akiongelea kuhusu imani za Kishirikina ambazo zilkuwa katika Vinywa vha watu kuwa wanawake hawaruhusiwi kufa nya kazi za kiuchimbaji wa madini kutokana na jinsi yao, alisema kuwa hizo  ni imani potofu na kuongeza kjuwa kwa sasa hata wao wamekuwa wakizama katika mashimo na kuchimba kama wachimbaji wengine.

Alisema kuwa imani hizo ni fikra potofu ambazo zipo kwa watu ambao hawana upeo wa Maisha na kuongeza kuwa wanawake na migodi hakuna maahusiano yeyote yale mabaya na hizo ni utaratibu mbaya ambao waatuo wamejiwekea.

Kwa upande wake Afisa madini mkazi Arusha Bertha Luzabuka amesema kuwa amewaasa wana wake haswa kutoka katika sekta ya madini kuendelea kuchangamkia fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta ,kuwa wabunifu hiyo haswa kwenye kuongezaji thamni wa madini ya vito,utengenezaji wa bidhaa za usonara,kwani Taifa linahitaji vitu vingi vunavyotokana na madini.

‘’Madini haya yanaweza kuongezewa thamani na yakatengeneza bidhaa nyingine mbalimbali ‘ukiangalia kaulimbiu ya siku ya wanawake duniani inaosema wanawake na wasichana 2025 tuimarishe haki usawana uwezeshaji ninawaasa wanawake wote tuendelee kushikamana kuwa wabuni fukatika sekta ya madini,taifa linahitaji vitu vingi vinavyotokana na madini hivyo tuweke vikundi na tushirikishane mawazo mbalimbali namna ya kuongeza thamani ili uweze kukuza vipato na kuendeleza familia zettu n Taifa kwa ujumla. alisema  Bi Bertha

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Wachimbaji Wanawake Mkoa wa Kagera (KAWOMA) Amina Mtiliga alisema kuwa changamoto kubwa ambayo imekuwa ikiwakuta wachimbaji wanawake ni pamoja na kukosa mitaji ya kuchimbia.

Alisema kuwa kutoka ana na kuwa na mitaji midogo wanakuwa hawapati fursa ya kuchimba kwani kazi hiyo inahitaji kuwa na zana bora za kisasa pamoja na fedha nyingi hali ambayo wanamuomba Rais WA Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hasssani kuona jinsi ya kuwawezesha ili waweze  kufanya kazi hiyo

‘Wanawake tumekuwa tukichimba madini na tunapata  pesa hila mitaji yetu ni midogo, tunamuomba Rais Samia Suluhu Hassani kuanghalia jinsi ya kutuwezesha  kwani wanawake kwa sasa kimbilio letu katika sekta ya madini serikali kuweka ngvu ili nasi tuweze kufanikiwa katika sekta hiyo”, Alisema Amina Mtiliga.

Kilele cha siku ya Wanawake Duniani kwa hapa nchini inatarajiwa kufanyika kitaifa katika mkoa wa Arusha huku Mgeni Rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Sulkuhu Hassani siku hiyo.

Mwisho

 

 

 

 















No comments