VIONGOZI SMAUJATA ARUSHA WAFUNDWA

Katibu Mkuu wa Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii (Smaujata)nchini Mhandisi Juliana Marko akizungumza na Viongozi ww Wilaya pamoja na wale wa mkoa alipotembelea katika mkoa huo katika katika shughuli sake za kikazi kushoto kwake ni Mwenyekiti wa mkoa wa Arusha Godfrey Zablon
Katibu Mkuu Smaujata akisaini Kitabu cha wageni

Baadhi ya Viongozi Smaujata Mkoa ww Arusha wakiwa katika kikao na Katibu Mkuu Samaujata Taifa
Katibu Mkuu Smaujata Taifa wa pili kutoka kushoto Juliana Marko akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Arusha mapema Leo Marchi 27/3/2024
Baadhi ya Viongozi wa Smaujata mkoa wa Arusha wakiwa katika kikao kilichofanyika Jijini Arusha Leo Marchi 27,2023 
Katibu wa Smaijata Lussa Melembu akitoa ripoti ya utendaji kazi kwa Katibu mkuu Smaujata
Katibu Mkuu Smaujata Taifa akiwasili katika kikao Mkoani Arusha. picha zote na Vero Ignatus. 
VIONGOZI SMAUJATA ARUSHA WAFUNDWA

Na. Vero Ignatus, Arusha

Katibu Mkuu mtendaji wa Smaujata amewataka Viongozi kusimamia vyema nafasi walizonazo sambamba na  kuwa barua njema kwa kila anayewasoma

Ameyasema hayao katika kikao cha Viongozi wa Smaujata mkoa kilichofanyika Jijini Arusha, ambapo aliwataka kutambua kuwa Uongozi ni majukumu poa ni mgumu,kwani hawawezi kupendwa na kila mtu badala yake kila mmoja  wao atambue nafasi yake, waitumikie jamii kwa moyo wa huruma,kwa kusimamia haki, pamoja na kuwa na kifua cha kubeba mambo. 

Aidha aliwataka Viongozi hao wajitahidi kuwa waadilifu kwenye nafasi zao, watafute namna wanaweza kutengeneza utaratibu wa kufuatilia mambo pamoja na kutoa nafasi kwa wengine, zaidi kufahamu mipaka yao ya kiutendaji. 

"Ninyi kama Mashujaa na Viongozi ni vyema kutambua kwa kupitia uzoefu wa namna moja ama nyingine mnaweza kuangalia namna gani njema ya kutatua changamoto"alisema Injinia Juliana

Akisoma ripoti ya utendaji wa kazi katika mkoa Kaimu Katibu wa Smaijata 
Lussa Melembuki alisema kuwa hadi sasa wameweza kufikia jumla ya shule za msingi zaidi ya  246,shule za sekondari zaidi ya 118,Makanisa 42,  wamefanya semina 12 pamoja na kushiriki zaidi ya matamasha 18 vyote hivyo ni kwaajili ya outta elimu kwa jamii dhidi ya Ukatili

Vile vile ameweza kuushukuru Uongozi wa seriali ngazi ya mkoa kwa kuwapatia ushirikiano mkubwa kwani wamekuwa sababu ya wao kufanikisha kutoa elimu katika jamii, ikiwemo kuwajuza madhara yatokanayo na Ukatili, na mahali sahihi pa Kutoa taarifa endapo wataona dalili ama jambo lolote lenye viashiria vya ukatili. 

Aidha ifahamike kuwa Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania ni kampeni mahususi ya Kitaifa kwaajili ya kupinga, kuibua na kutokomeza vitendo vyote vya ukatili katika Jamii zote nchini, kuelimisha Jamii kuondokana na fikra, Imani, Mila na desturi na tamaduni zinazokinzana na Maendeleo. 

Baadhi ya malengo ya kampeni hii ni kutambua kutengeneza mtandao Jamii, sense uwezo wa kupaza Sauti kupinga nakupambanaa na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na Watoto, kuelimisha na kurahisisha utambuzi na ufanyiaji kazi viashiria vyote vya ukatili kuanzia ngazi ya Familia.. 






No comments