Na.Vero Ignatus,Arusha
DKT.MWIGULU :PSPTB KAZI HII NI YA KIZALENDO WAPENI WATANZANIA
Taarifa ya utendaji ya PSPTB imesema kuwa ipo changamoto kubwa ya baadhi ya wataalamu waliobainika kufanya kazi pasipokuwa na sifa stahiki na bila kusajiliwa na bodi kama ilivyo takwa la kisheria kifungu cha sheria cha PSPTB,kwani inachangiwa na waajiri kuruhusu kazi za ununuzi kufanywa na waajiriwa nje ya taaluma ya ununuzi na ugavi ambayo kwa ukubwa wake imeinazigusa ofisi YA Rais Tamisemi yenye watumishi wengi zaidi wa kada hiyo
Hayo yamesemwa leo Jijini Arusna na Waziri wa fedha Dkt.Mwigulu Nchemba katika kongamano la la mwaka la wataalam wa ununuzi na ugavi,ambapo amemuelekeza katibu mkuu wa wizara ya fedha kushirikiana na Bodi kukutana na Katibu Mkuu Tamisemi ,Katibu mkuu Utumishi wa Umma kwa utatuzi wa changamoto hiyo ili kuhakikisha kazi za ununuzi na ugavi zinafanywa na wataalam wenye sifa nz waliosajiliwa na bodi hiyo kwa mujibu wa sheria ya PSPTB
Dkt Mwigulu amesema pamoja na kutambua juhudi za PSPTB katika kusimamia taaluma ya ununuzi na ugavi amepokea changamoto ya maslahi madogo kwa wataalam haswa wanaohitimu cheti cha kitaalam cha CPSP ukilinganisha na taaluma zingine kama uhasibu na sheria
“Serikali inatambua kuwa ununuzi unachukua sehemu kubwa ya bajeti ya serikali na hivyo mchango wawataalam hawa lazima utahaminiwe ili wataalam waweze kufanya kazi bila vishawishi”alisema Dkt.Mwigulu
Akinukuu kutoka kwenye taarifa ya utendaji Dkt.Mwigulu amesema kuwa pamoja na changamoto ya maslahi imeeelezwa kuwa PSPTB imekuwa na changamoto ya utekelezaji wa baadhi ya majukumu yake kisheria ikiwa ni pamoja na kufanya ukaguzi wa wataalam wake nchini nzima,katika sekta umma,binafsi ,kuwajengea uwezo wataalam na wadau kwenye mnyororo wa ununuzi na ugavi na kufanya utafiti wa kitaalam ili kuleta ufumbuzi wa usimamizi bora wa mnororo wa ununuzi na ugavi kwasababu ya ufinyi wa bajeti
Hivyo amemuagiza Katibu Mkuu wizara ya Fedha kuangalia uwezekano wa kuisaidia PSPTB Kupata fedha kufanikisha majukumu hayo,Vilevile Dkt.Mwigulu amewataka psptb kuwapatia watanzania kazi ili waweze kuwaajiri wageni siyo kila mara wageni ndiyo wanawaajiri wazawa kwa kutumiataaluma na ujuzi wao kasha wanaandika ripoti kwa kutumia utendajikazi wa Watanzania
“Kazi hizi ni zakufanya kizalendo wapeni watanzania kazi,kasha wao wawape wagenikazi jamani,wekeni upendeleo kwa wenye nchi yao,nchi tajiri zote duniani uchumi wake unashikiliwa na sekta binafsi “alisema
Aidha itakumbukwa kuwa katika hotuba ya wizara ya fedha iliyosomwabugeni ya mwaka 2023/2024 ilitoa dira ya hotuba ya serikali kuhakikisha ununuzi unafanyika kwa njia ya mtandao kwa kuzingatia bei halisi ya soko ili kupunguza gharama katika ununuzi wa umma na kuleta tija kw aTaifa katika utekelezai wa mnyorororo wa ununuzi wa ugavi nchini
Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa PSPTB Jacob Jail Kibona katika kongamano hilo ametaja baadhi ya mafanikio ambayo yamepatikana tangia kuundwa kwa bodi kwa sheria ya bunge namba 23 ya mwaka 2007 ,amesema bodi hiyo imefanikiwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa kifungu cha 7 cha psptb kwa kusimamia kukuza fani ya ununuzi na ugavi nchini,ambapoimeendelea kuuhisha mitaala ya mafunzo ya kitaalam na kuzalisha wataalam wenye ujuzi na umahili.
Aidha PSPTB imeendelea kudhibiti ubora wa taaluma kwa kupitia mitaala ya vyuo na taasisi nyingine zaelimu ya juu zinazotoa mafunzo ya fani ya ununuzi na ugavi nchini sambamba na kuendesha mitihani ya kitaaluma kwa watahiniwa katika fani ya stashahada ya kitaalam na stashahada ya kitaalam ya cheti cha kitaaluma cha juu kwa wanaofanya kazi ya ununuzi na ugavi
Kongamano hilo la 14 la
mwaka la wataalam wa ununuzi na ugavi
limebeba mada isemayo mabadiliko ya kidijitali katika kuboresha usimamizi wa
mnyororo wa ununuzi na ugavi kwamaendeleo endelevu
No comments