WIZARA YA FEDHA /WADAU WA SEKTA YA FEDHA NCHI WAANDAA MAONYESHO TATU YA HUDUMA ZA KIFEDHA JIJINI ARUSHA
WIZARA YA FEDHA /WADAU WA SEKTA YA FEDHA NCHI WAANDAA MAONYESHO YA TATU YA HUDUMA ZA KIFEDHA JIJINI ARUSHA
Maadhimisho
ya tatu wiki ya huduma za fedha Kitaifa yameanza rasmi leo Jijini Arusha 20/11/2023 ambapo yameamdaliwa na Wizara ya Fedha
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya fedha nchin, ikiwa ni utekelezaji
wa mpango mkuu wa maendeleo ya sekta ya Fedha wa mwaka 2020/21-2029,kipaumbele
kikiwa ni kutoa elimu kwa umma katika utekelezaji wa mpango huo sambamba na
kupunguza umaskini.
Akizungumza
na waandishi wa Habari Jijini Arusha Kamishna wa Idara ya uendelezaji wa Sekta
ya fedha Dkt.Charles Mwamwaja juu ya maaadhimisho hayo ,alisema kuwa Tanzania
ifikapo mwaka 2025 asilimia 80%watakuwa wamepata uelewa wa huduma za kifedha
ikiwemo benki masoko na dhamana za mitaji huduma za bima ,huduma za mifuko ya
uwezeshaji wananchi kiuchumi
Amesema
serikali kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya fedha inajitahidi kuhakikisha
kuwa wa wawe wamefikiwa na huduma hizo kwa kutoa elimu ya umuhimu wa
matumizi ya huduma hizo.
Alisema kuwa
kutokana na utafiti wa Finscope wa mwaka 2023 nchini ni asilimia 53.8 tu ya
nguvu kazi wanatumia rasmi huduma rasmi za fedha ambapo kundi kubwa la
watanzania halifaidiki na huduma hizo na kusababisha kukosa fursa za kuboresha
Maisha kupitia shughuli mbalimbali za kiuchumi ambazo zingewawezesha kukuza na
kuchangia pato la Taifa.
Dkt.Mwamwaja
amesema kuwa malengo ya wiki hiyo ya huduma ya kifedha ni pamoja na Kujenga
uelewa na weledi kwa umma katika matumizi sahihi ya huduma za kifedha ili kujenga uchumi na kuondoa umaskini,
Kuimarisha ufanisi wa Masoko ya Fedha kupitia elimu ,Kuongeza upatikanaji wa
huduma jumuishi,, Kutoa elimu ya kumlinda mtumiaji wa huduma,Kuwezesha wananchi
kusimamia vizuri rasilimali fedha,kuwezesha wajasiriamali wadogo kuongeza ujuzi na
matumizi sahihi ya huduma za kifedha katika kukuza biashara zao.
‘’Maadhimisho
hayo ni pamoja na mambo mengine yanalenga kuwajengea wananchi huduma ya uelewa
kuhusu matumizi sahihi ya huduma za kifedha sambamba na Kuimarika kwa utamaduni wa kujiwekea akiba,
kukopa na kulipa madeni,na Kuongezeka kwa mchango wa Sekta ya Fedha kwenye
ukuaji wa uchumi’’.Alisema Dkt.Mwamwaja.
Dkt.Mwamwaja
aliongeza kuwa maadhimisho hayo yanalenga kuwaunganisha wananchi wajasiriyamali
na wadau wengine ili waweze kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na sekta hiyo
ya fedha katika kuimarisha na kukuza biashara zao sambamba na kuwakaribisha
wananchi kushiriki kwani hakuna kiingilio.
‘’Niseme kwamba Njia mbalimbali tutakazotumia katika kutoa elimu ya fedha kwa umma ni pamoja na machapisho(vipeperushi, na mabango madogo); uandishi wa insha; gari la matangazo; semina; maonesho ya bidhaa za fedha; majukwaa ya kidigitali(mfano; simu za kiganjani), mitandao ya kijamii, vyombo mbalimbali vya habari(TV, Radio, Magazeti) pamoja na burudani’’Alisisitiza Dkt.Mwamwaja
Maadhimisho
hayo ya tatu ya wiki ya huduma za kifedha yaanaanza leo katika Viwanja vya Shekh
Amri Abeid Jijini Arusha yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa siku ya jumatano tarehe 22/11/2023
No comments