BORESHENI HUDUMA PAMOJA NA KUTUMIA MUDA MFUPI KWA WATEJA WENU/WAGENI WANAOHITAJI FAFANUZI MBALIMBALI ZA KIMTANDAO

Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom katika Duka jipya lililofunguliwa leo katika eneo la AIM MALL jijini Arusha wakimuhudumia mteja Raia wa kigeni aliyefika akihitaji huduma
Katika picha ni baadhi ya wateja wakipatiwa huduma katika Duka jipya la Voda Shop lililofunguliwa Mei 26 2023 Aim Mall Jijini Arusha 
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mtahengerwa akikata keki kama ishara ya ufunguzi wa Voda shop Aim Mall Jijini Arusha kushoto wake ni Fevis Christian Mkurugenzi wa Voda shop Aim Mall.
Shamrashama zikiendelea maa baada ya uzinduzi wa Voda Shop AIM MALL jijini Arusha 
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtahengerwa akikata keki kama ishara ya ufunguzi wa Voda shop Aim Mall Jijini Arusha kushoto wake ni Devis Christian Mkurugenzi wa Voda shop Aim Mall.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtahengerwa akizungumza na wananchi waliohudhuria hafla hiyo fupi ya uzinduzi kushoto wake ni Devis Christian na kulia kwake ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini , George Venanty 

Wateja wakiendelea kupatiwa huduma katika Voda Shop iliyofunguliwa AIM MALL Jijini Arusha mei 26 2023

BORESHENI HUDUMA PAMOJA NA KUTUMIA MUDA MFUPI KWA WATEJA WENU/WAGENI  WANAOHITAJI FAFANUZI MBALIMBALI ZA KIMTANDAO

Na Veronica Ignatus, Arusha

Kampuni ya simu ya Vodacom  inazojihushisha na utoaji wa huduma za mawasiliano kwa wananchi na wageni waingiao nchini  imetakiwa  kuboresha huduma zake ikiwemo kutumia muda mfupi kuhudumia wateja mbalimbali waonataka kupata ufafanuzi wa huduma mbalimbali za kimtandao ikiwemo utalii mbugani

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtahengerwa  katika uzinduzi wa duka lao jipya katika eneo la lAim Mall Jijini Arusha,ambapo umekwenda sambamba na kukabidhi hundi ya sh,milioni 5.5 kwa mshindi wa bahati nasibu ya Tusua Mapene kwa ndugu Matei Tarimo

Aidha  Mtahengerwa ambaye alisititiza kuwa ,Mhe,Rais Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa katika filamu ya Royal Tour ambayo imeongeza idadi ya utalii,hivyo ni vyema kuzingatia maadili na lugha njema,kwani filamu hiyo imepelekea shughuli za utalii kukua ikiwemo huduma za mawasiliano haswa vijijini. 

"Hivi sasa watalii ni wengi lakini nawaomba Vodacom mboreshe huduma zenu za mawasiliano lakini pia boresheni kitengo cha huduma kwa wateja kwa kuwahudumia muda mchache,"

Kwa upande wake  Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini , George Venanty amesema kampuni hiyo umekuwa mstari wa mbele kusogeza huduma kwa wateja kwa ukaribu kwani Arusha ni mji wa utalii,ambapo hivi sasa wanamaduka zaidi ya 66 Jijini Arusha.

Venanty ametoa wito kwa wateja wa vodacom waendelee kushiriki katika bahati nasibu zilizopo ili wajishindie zawadi mbalimbali alitoa rai kwa wateja mbalimbali kumtembelea maduka yao ili wapate huduma mbalimbali ikiwemo kasi ya mitandao ya 5G.

Duka hilo linatoa huduma mbalimbali ikiwemo usajili wa laini za vodacom,simu janja ,huduma za m-pesa,kutengeneza lipa namba na huduma nyinginezo

kwa upande wake Mshindi wa tusua mapene,Matei Tarimo amesema alishukuru kampuni hiyo kwa kumpa hela hizo ambazo zitamsaidia kujikwamua kiuchumi

No comments