SHIRIKISHO LA WATU WENYE ULEMAVU:MTUMIZI YA LUGHA YA ALAMA YATILIWE MAANANI KATIKA SHUGHULI MBALIMBALI ZA KIJAMII
Wakwanza kulia ni Mwenyekiti wa CHAVITA bi Selina Mlemba,akifuatiwa na Katibu Mkuu wa shirikisho la watu wenye ulemavu Jonas Lubalo wakitoa ufafanuzi kwa vyombo vya habari juu ya maadhimisho ya siku hiyo
Katibu wa kanisa la watu wenye ulemavu Joseph Hiza:tunahitaji wakalimani wa Lugha ya Alama kwenye maeneo mengi kwani hata sisi tunahaki ya kupata taarifa.
SHIRIKISHO LA WATU WENYE ULEMAVU:MTUMIZI YA LUGHA YA ALAMA YATILIWE MAANANI KATIKA SHUGHULI MBALIMBALI ZA KIJAMII
Na.Vero Ignatus,Arusha
Kaika kuelekea siku ya Kimataifa ya watu wenye ulemavu Duniani Desemba 3, Shirikisho la watu wenye Ulemavu kwa kushirikiana na Chama cha viziwi nchini Tanzania (CHAVITA)imeiomba Serikali, vyombo vya Habari kutekeleze sheria ya mawasiliano na Posta, kuhakikisha matukio yote muhimu yanakuwanna wakalimani wa Lugha ya Alama
Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Arusha ,Mwenyekiti wa CHAVITA bi Selina Mlemba amesema kuwa maadhimisho hayo hulenga kukuza uelewa na kuhamasisha mahitaji muhimu yanahusishwa na watu wenye Ulemavu(WWU)na kujumuisha kundi hilo katika jamii na michakato ya maendeleo.
Mlemba amesema kuwa vyombo vya habari vina jukumu muhimu kwa jamii kwa kufichua changamoto za kijamii kwa kusambaza taarifa,kuelimisha,kusaidia kufikisha sauti kwa viongozi na wengine wenye Mamlaka.
"Hata hivyo wakati Watanzania waielekea kuadhimisha miaka 61 ya uhuru bado yapo mambo mengi ambayo hayajatekelezwa na Mamlaka husika ikiwemo mkataba wa Kimataifa wa Haki za WWU (UNCRPD) .Alisema Mlemba
Nae Katibu wa kanisa la watu wenye ulemavu Joseph Hiza amesema kuwa miongoni mwa maeneo ambalo halijapewa kipaumbele na vyombo vingi vya habari haswa televisheni ni utekelezaji wa sheria ya Posta na Mawasiliano kifungu cha 38(1)(a)ambacho kinazungumzia umuhimu wa ufikivu wa mawasiliano kwa jamii ya Viziwi nchini Tanzania.
Amesema matatizo mengi ya viziwi ni katika mawasiliano,hivyo hayaonekani kwa macho kwani wamekuwa wakibaguliwa na tatizo la kushaulika katika mipango,sera na utoaji wa huduma mbalimbali katika mazingira wanamoishi hivyo humwathiri kwa katika nyanja ya elimu,mahusiano na maendeleo ya jamii.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa shirikisho la watu wenye ulemavu Jonas Lubalo amesema changamoto ya lugha ya alama kutopewa uzito, imeanzia kwa viongozi kitaifa na kushuka chini hadi ngazi ya familia na hii ni kutokana na lugha hiyo kupuuzwa na kutowekwa daraja moja na lugha nyingine tofauti na mataifa mengine ya jirani .
Jonas anasema Mawasiliano ndiyo nyenzo namba moja katika suala zima la maendeleo, ambapo na sisi tunahitaji kuwa sehemu ya hayo maendeleo,aidha
Tanzania inatajwa kuwa nchi ambayo yenye wakalaimani wachache wa lugha ya alama jambo ambalo inaonekana kuwatenga watu wenye ulemavu hiyo
" Karibu hotuba zote za viongozi hazihusishwi wakalimani wa lugha ya alama ,mbaya zaidi mara chache tumekuwa tukipewa viporo tena nyakati ambapo ziyo sahihi,hata hotuba ya Rais wetu haihusishi mkalimani kana kwamba Amir Jeshi Mkuu wa Taifa letu siyo kiongozi wetu alisema.
Aidha siku ya Kimataifa ya watu wenye Ulemavu Duuniani itafanyika Jijini Arusha ikiwa imebeba Kauli mbiu inasemayo "Suluhisho la Mabadiliko kwa Maendeleo Jumuishi :Nafasi ya Ubunifu katika Kuchagiza Dunia fikivu yenye Usawa.
No comments