TMDA YASHIRIKI KUSANYIKO LA KISAYANSI SADC JUU YA UDHIBITI WA UHAI WA DAWA
Prof.Peter Iming kutoka chuo Kikuu cha Martin Luther nchini Ujerumani,akizungumza katika Warsha kusanyiko la kisayansi na wataalam juu ya udhibiti wa uhai wa dawa katika eneo la nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara Wa kwanza kushoto Titus Malulu Mkaguzi wa Dawa na Mtaalam wa Maabara akiwa na baadhi ya wageni waliofika kwenye kusanyiko la Kisayansi liilofanyika Jijini Arusha,wakiwa katika ofisi ya Kanda ya kaskazini TMDA ambavyo maabara hamishika inavyofanya uchunguzi wa dawa. Wakwanza kulia ni Prof.Peter Iming kutoka chuo Kikuu cha Martin Luther nchini Ujerumani,akifuatiwa na Prof.Lutz Heide kutoka chuo kikuu cha Ufamasia nchini Ujerumani,akifuatiwa na Mkurugenzi wa Vifaa Tiba na Vitendanishi (TMDA) Kissa Mwamwitwa,Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Muhimbili (MUHAS) Prof.Dkt.Eliangiriya Kaale,kushoto kwake ni Meneja wa Kanda ya Kaskazini TMDA Proches Patrick,wakifuatilia namna ambavyo maabara hamishika inavyotambua ubora wa dawa
NA.VERO IGNATUS,ARUSHA
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imeweza kushiriki katika kusanyiko la Kisayansi la siku tano juu ya Udhibiti wa uhai wa dawa katika eneo la nchi za kusini mwa jangwa la Sahara (SADC) lillofanyika Jjijini Arusha ,kupitia Mradi wa Maarifa ya Kesho.
Akizungumza Mkurugenzi wa Vifaa Tiba na Vitendanishi (TMDA) Kissa Mwamwitwa ambaye pia alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu amesema kuwa lengo la kusanyiko hilo ni kujadili mnyororo mzima kuanzia uzalishaji wa dawa,hadi utupaji salama na uondoaji wa kemikali za dawa katika mfumo wa maji taka mara dawa zinapomaliza muda wake na kuteketezwa.
Mwamwitwa alisema katika Kongamano hilo la Kisayansi waliweza kuangalia jinsi gani wanatumia maabara inayohamishika, katika kufanya uchunguzi wa kimaabara kuangalia ubora wa dawa ,hususani katika vituo vya forodha na katika ofisi za Kanda za TMDA,ambapo dawa yeyote inayoingia nchini wanachukua sampuli na kuweza kuangalia ubora
‘’Kwahiyo Mamlaka hii ya Dawa na Vifaa Tiba inawajibu mkubwa wa Udhibiti wa dawa,kuangalia ubora na ufanisi kabla hazijaingia sokoni na baada ya kuingia sokoni, wanamlinda Afya ya mwananchi na kuhakikisha wanatumia dawa zilizo salama na zenye ufanisi’’tukishajiridhisha na ubora ndipo dawa inaendelea kutumika pamoja na kuchukua sampuli, tunahakikisha kuwa bidhaa zote ni bora na zenye ufanisi kwaajli ya matumizi’’Alisema.Mwamwitwa.
Profesa Eliangirika Kaale ni Mtafiti kutoka Chuo Kikuu na Sayansi na Afya Shirikishi Muhimbili(MUHAS) : Tumeshirikishana uzoefu kutoka kwa kila mmoja wetu ambapo tumeona kuwa Mkakati wa kwanza ni kupunguza kusiwepo na dawa za kuharibu,kwa maana ya kwamba ni jinsi gani tutaepuka matumizi ya dawa ili mwisho wa siku kusiwepo na dawa nyingi ambazo zinabakia kwaajili ya kutupwa au kuteketezwa.
‘’Kwa upande wetu kwa sasa kuna changamoto kubwa ya safe disposal ya dawa kwasababu wadau mbalimbali hawajashirikishwa ,hivyo sisi kama watafiti wameona ni vyema wakawaleta kila wadau wanaohusika kwenye mnyororo huo wakiwemo walaaluma,wadau kutoka viwandani na Mamlaka za uthibiti’’.Alisema Kaale
Kaale:Tumekaa pamoja tukajadili kila mmoja
wetu kwenye huu mnyororo kuanzia dawa iapoanza kutengenezwa mpaka dawa
inavyotupwa ,na tumeweza kuja na
mkakati kitu gani tunaweza kwenda kufanya
ili kuhakikisha kwamba dawa ikishamaliza muda wake ni jinsi gani
zitaharibiwa katika njia ambazo hazitaathiri mazingira
Kwa upande wake Prof.Peter Iming kutoka chuo Kikuu cha Martin Luther nchini Ujerumani,alisema amefurahishwa kuwa sehemu kusanyiko hilo la kisayansi la nchi za kusini mwa jangwa la Sahara SADC ,kwani wamefanya mjadala mkubwa ambapo utaleta matokeo chanya haswa kwenye uzalishaji,utupaji na uondoaji wa kemikali katika mfumo wa majitaka
Amesema wameweza kubadilishana uzoefu kutoka katika nchi mbalimbali na yeye kujumuisha na zile za nchini kwake na kuona kwamba mjadala huo umekuwa wa tija na umewaleta pamoja kuona namna ambayo wanaweza kutatua changamoto iliyopo kabla tatizo halijawa kubwa na kuleta madhara kwa mazingira na kwa binadamu.
chini ya ufadhili wa Taasisi ya VW Foundationpamoja na mradi huo unaofahamika kwa jina la Maarifa ya Kesho(Knowledge for tomorrow), pamoja na miradi Shirikishi ya Tafiti katika eneo la nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara.

No comments