JAMII IHUSIKE KUHAKIKISHA WANAWAKE WANAPATA NAFASI ZA UONGOZI WA KISIASA KATIKA NCHI ZAO
Ndagiza Anastazia Wambura mbunge viti maalum kutoka mkoa wa Mtwara wakati
akifungua mkutano wa viongozi wanawake unaoendelea mkoa Arusha katika
makao ya jumuiya ya Africa mshariki kwa niaba ya spika wa spika wa Bunge
la jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Tulia AcksonAgnes Sadiki mmoja wa wanaharakati wanaopigania haki za wanawake kutoka Congo
DRC ambaye pia alishawahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo kuwa waziri wa uchukuzi nchini humo ikiwemo kuwa msemaji
wa serikali na waziri wa bajeti
Dkt Rebecca Kadaga Waziri wa Jumuiya ya Africa Mashariki kutoka Uganda alisema kuwa amekuwa spika wa Bunge la Uganda kwa miaka kumi
NA.VERO IGNATUS ARUSHA
Mila,
desturi na tamaduni ambazo zinawaona wanawake ni viumbe duni,hawawezi kutoa maamuzi, imetajawa kuwa kikwazo cha wanawake kukabiliwa na changamoto mbalimbali ,
zinazozuia wao kuingia katika nyanja za siasa pamoja na uongozi, ikiwemo
kukabiliwa na shughuli nyingi za kifamilia,ambapo Jamii ikihitajika kuhusika kuhakikisha wanawake wanapata nafasi za kisiasa.
Hayo yamesemwa na Anastazia
Wambura mbunge viti maalum kutoka mkoa wa Mtwara wakati akifungua
mkutano wa viongozi wanawake unaoendelea mkoa Arusha katika makao ya
jumuiya ya Africa Mshariki kwa niaba ya spika wa Bunge la
jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson na kuwataka Wanawake
kutoka nchi mbalimbali za Kanda za Afrika ikiwemo EAC, SADIC, COMESA na
ECOWAS,kuwania nafasi mbalimbali za uongozi
katika nchi zao
''Mambo kama haya ndo yanaenda kujadiliwa
lakini pia kubadilishana uzoefu kati ya nchi na nchi kuona wao
wamewezaje kwa mfano Rwanda utaona wao wako karibia asilimia 64 ya
wabunge ni wanawake lakini kwetu Tanzania ni asilimia 37 na wapo ambao
wapo chini ya hapo hivyo tutabadilishana uzoefu”Alisema
Mhe.Wambura alisema kuwa ni vema wanawake wakapata nafasi za uongozi kwani mwanamke ndiye mzazi,mlezi, mtu mwepesi wa kubaini matatizo katika jamii pamoja na chombo kikubwa Cha amani,Japokuwa majukumu yake mengi katika Jamii yanamkosesha muda wa kujishughukisha na masuala ya siasa.
“Tutaangalia kwa pamoja tufanyeje ili tuweze kuhakikisha kwamba wanawake Afrika wanapata nafasi za uongozi kwani tunataka tuwe asilimia 50 kwa 50 lakini kwasababu ya hizi changamoto ndio maana bado hatukafikia lakini pia ni nafasi za wakereketwa kuhakikisha kwamba nafasi za wanawake zinaongezeka, bado nchi nyingi hazijawaweza kuweka kwenye mitaala lakini ni mapendekezo,” Alisema.
“Kwamba watoto wanapoingia darasa la kwanza hadi la saba wajue kuwa mwanamke ni mtu wa muhimu katika kuiendeleza jamii kwahiyo wasiwe na mtadhamo hasi dhidi ya mwanamke, watakapowekewe kwenye mtaala moja kwa moja akiwa mkubwa akiambiwa nenda kapige kura anakuwa akijua niliambiwa kuwa mwanamke ni kiumbe muhimu katika kuleta maendeleo kwenye jamii,” Alieleza.
Agnes Sadiki ni mmoja wa wanaharakati wanaopigania haki za wanawake kutoka Congo
DRC ambaye pia alishawahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo kuwa waziri wa uchukuzi nchini humo ikiwemo kuwa msemaji
wa serikali na waziri wa bajeti, anasema kuwa amefurahi kuona nchi nyingi
zinaendea kupiga hatua katika kuwashirikisha mwanamke katika ngazi za
uongozi na kutolea mfano Tanzania Zambia na Rwanda.
“Itatubidi
katika nchi yetu ya Congo kuomba wakuu viongozi ambao nao wamesaini
mikataba mbalimbali ikiwemo ya protocoli ya Maputo na nyinginezo ambazo
zinaomba kumshirikisha mwanamke katika kila kitu ambacho kina lenga
amani kwasababu hakuna uongozi bila amani lakini pia katika chaguzi
kwani Congo tunajitahidi kuwa nchi yenye demokrasia,” Alisema.
“Tutaenda
katika uchaguzi hivi karibuni kwahiyo ni sharti wakuu viongozi kama
walivyosaini ile mikataba na kukubaliana kumweka mwanamke katika ngazi
ya uongozi waweze kuzitekeleza lakini inabidi pia wanawake wao wenyewe
wafanye juhudi za kuingia katika uongozi kwani wanastahili kuongoza
pamoja na wanaume lakini pia watambue kuwa hawataweka tu kwa sababau ni
wanawake bali wawe wanawake wanaostahili,” Alisema .
“Wawe
wanawake wenye ujuzi, wasomi, wamelimika lakini vilevile awe na
jitihada ya yule ambaye anastahili kuongoza kwa niaba ya wananchi kwa
faida ya akina mama na raia wengine,” Aliongeza.
Dkt Rebecca Kadaga ni Waziri wa Jumuiya ya Africa Mashariki kutoka Uganda alisema kuwa amekuwa spika wa Bunge la Uganda kwa miaka kumi hivyo yupo katika mkutano huo kubadilishana uzoefu nini wafanye ili wanawake waweze kupata nafasi za uongozi ikiwemo kukagua mambo mbalimbali ya serikali ikiwemo bajeti na uwakilishi wa wanawake kwa kuhakikisha asilimia 30 wanashiriki.
“ Tunataka kuhakikisha kuwa katika maeneo yetu kunakuwa na shule sahihi kwaajili ya watoto wa kike kwahiyo tupo kushauri kuhakikisha tunapaza sauti kwa pamoja na kufikia malengo ya kidunia katika nchi zetu za kuleta usawa katika mambo mbalimbali ikiwemo nafasi za uongozi,”Alisema.
Naye
katibu mkuu wa umoja wa wanawake wa Bunge la jumuiya ya Africa mshariki
(EALA) Fatma Ndagiza alisema kuwa mkutano huo ni wa siku tatu ambapo
lengo ni kuwapa nafasi wanawake waliopo katika siasa nafasi na
kubadishana mawazo na uzoefu hasa jinsia gani walifika katika nafasi
walizonazo zinazotoa uamuzi, kuelezana changamoto na ninamna gani
wataweza kuzikabili changamoto hizo.
“Tunatarajia
kuwa baada ya mazungumzo haya tutakuwa na mikakati mbalimbali ikiwemo
ya kujitahidi kubadili Katiba za nchi zetu au kama wawakilishi tuweze
kufuatilia na kuhoji serikali zetu ili wanawake wawe na mchango kwa
maendeleo ya taifa zao lakini pia wawe na wanawake wengi katika ngazi za
siasa,” Alisema.
No comments