IJUE OFISI YA MSULUHISHI WA MIGOGORO YA BIMA (INSUARANCE OMBUDSMAN)

Na.Vero Ignatus Arusha

''Kila robo mwaka tunapokea na kusuluhisha migogoro takribani 60,ambapo tokea mwaka 2021 umeanza hadi 23nov 2021 tumepokea migogoro 175 ambayo tumefanikiwa kwa 90% kuisukuhisha , bado migogoro michache ambayo tumeipata hivi karibuni tunaendelea na taratibu za kuisukuhisha''anasema Magreth Mngumi 

Ofisi  ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima ,ni Taasisi iliyoanziishwa chini ya sheria ya Bima namba 10 ya mwaka 2009 sura ya 394 ambapo ilianza kufanya kazi rasmi 2015 baada ya kuteuliwa kwa msuluhishi

Magreth Mngumi ni Msajili wa Malalamiko katika Ofisi ya Msuluhishi  wa migogoro ya bima,anasema Taasisi hiyo imeanzishwa chini ya sheria ya Bima, Sheria na 10 ya mwaka 2009 ,ambapo imeanza kufanya kazi mwaka 2015,inasuluhisha migogoro ya bima pale ambapo mwananchi anapoenda kudai fidia kwenye makampuni ya bima, asipopata huduma ambayo ataridhika nayo, badala ya kwenda mahakamani anatumia taasisi hiyo ili kubaini tatizo na litatuliwe kwa njia rahisi ambayo haina gharama.

Mngumi anasema Taasisi hiyo ni njia mbadala wa mahakama katika utatuzi wa migogoro ya bima,kwani  kwa Sasa  wanatumia Ofisi za Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini (Tira) katika Kanda mbalimbali kuweza kupokea migogoro ya bima pamoja na kuzitatua katika Ofisi hizo  yetu kwa kuhudumia Tanzania Bara na Zanzibar .

Hatua za usuluhishi kwanza Tunapopata mgogoro kutoka kwa yule ambae anaona hakutendewa haki, tuaiandikia Kampuni ya bima ili na yenyewe kuipa nafasi ya kusikilizwa, ili kujua kwamba tatizo ninini,tukishapata jibu la Kampuni hiyo,tunaitisha kikao cha usuluhishi tunakaa mezani na kuongea kwa uwazi kwa upana juu ya tatizo kililopo na kuweza kukitatua .

Mgumi amefafanua  malengo ya kuanzishwa kwa ofisi hiyo ni pamoja na kumlinda mtumiaji wa bima na soko, hivyo kujenga, kukuza imani ya umma kwenye biashara hiyo, sambamba na kutatuia migogoro kwa kutumia njia mbadala nje ya utaratibu wa kawaida wa kimahakama kwa haraka na kwa gharama nafuu

 Aidha njia zinazotumika kwaajili ya kushughulikia malalamiko kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazoendesha biashara ya bima ni pamoja na  sheria no 10 ya mwaka 2009,sheria ya bima za magari sura 169 kama ilivyorejewa 2002 ,sheria ya mikataba sura ya 345 kama ilivyorejewa 2002,kanuni za msuluhishi wa migogoro ya bima -GN411ya mwaka 2013 mikataba ya( insuarance policy) njia kuu za kutatua migogoro pamoja na upatanishi usuluhishi na uamuzi

Vilevile ili Ofisi ya msuluhishi wa migogoro iweze kushughulika na malalamiko ya mhusika, lazima aonyeshe kuwa ni mwathirika ambaye hakubaliani na uamuzi wa kampuni ya bima kuhusu madai yake au kiwango cha fidia stahiki,sambamba kupunjwa fidia,kucheleweshwa au kukataliwa kwa madai yote

Alisema mleta malalamiko yanaweza kuwasilishwa na malalamikaji mwenyewe akiwa ni mbima mwenyewe au mhanga wa ajali ambaye analindwa kisheria au mrithi ,mfaidika wa waliotajwa na mwakilishi aliyeidhinishwa kisheria,ambapo mud awa kuwasilisha ni ndani ya kipindi cha miaka mitatutangu tarehe ya mlalamikaji alipofahamu kuwa ana haja au sababu ya kuwasilisha malalamiko kwa msuluhishi

Malalamiko hayo yanaweza kuwasilishwa kwa maandishi barua ,barua pepe na yaelekezwe kwa msuluhishi wa migogoro ya bima,kwa njia ya kujaza fomu,ambayo iko katika kanuni za kusughulikia malalamiko ambapo fomu hiyo inapatikana katika Ofisi ya msuluhishi wa mogogoro ya bima na katika tovuti  www.tio.go,ambapo malalamikaji anatakiwa aweke wazi kiini cha malalamiko yake,pamoja na kuambatanisha nyaraka zote zinazohusu madai ya bima,nyaraka za mawasiliano kati ya mlalamikaji na mlalamikiwa

Vilevile Mlalamikaji anapaswa kulipa ada ya kusajili malalamiko kupokelewa na msajili ,kwa mijibu wa sheria na kanuni zilizoainisha ofisi ya msuluhishi wa migogoro ya bima kanuni ya 15 (5) ambapo mlalamikaji anapaswa kuwasilisha kwenye ofisi hiyo ya Msuluhishi ikiwa ni uthibitisho wa malipo ya ada kutoka bank na atapatiwa risiti

Mngumi alihitimisha kwa kusema kuwa, muda wa kushughulikia migogoro unapaswa kutatuliwa ndani ya siku 60 tangia tarehe ya kusajiliwa kwake,katika kuhakikisha hayo yanafanikiwa nyaraka muhimu zinazohitajika kuambatanishwa na barua ya lalamiko,mkataba wa bima ,fomu ya polisi no 93,90,na 115,ramani ya eneo la ajali ,hati ya mashtaka  hukumu,taarifa ya daktari,leseni ya dereva ,kadi ya gari picha ya muhanga ,risiti za matibabu na usafiri.

Ikumbukwe kuwa ,wahusika wakuu katika ofisi ya msuluhishi wa migogoro ya bima ni Msuluhishiwa migogoro ya bima mwenyewe,Msajili wa migogoro ,Afisa mthamini,Msuluhishi Mwandamizi na Muamuzi Mwandamizi

Mwisho

 

No comments