TAEC:ZINGATIA USALAMA KATIKA MAENEO KAZI JIKINGE NA ATHARI ZITOKANAZO NA MIONZI
Na.Vero Ignatus,Arusha
Wataalam wa wanayofanya kazi karibia ana mionzi wamepatiwa mafunzo maalum ili kujikinga na madhara yanayotokana na athari za mionzi
Akizungumza mkuu wa Idara ya uhifadhi ya mabaki ya vyanzo vya mionzi Salehe Mulisha ambae amemuwakilisha mkurugenzi mkuu wa TAEC aliwataka kutumia mafunzo hayo kujikinga na athari zitokanazo na mionzi
Amesema lengo kubwa ni kuwakumbusha Usalama wa kazi katika maeneo yenye vyanzo vya mionzi ,ambapo mafunzo hayo yanatoa Elimu ya kujikinga na Mionzi, kwani kufanya kazi bila kuzingatia Usalama ,kunaweza kuleta madhara makubwa kwa anaetumia sambamba na kwa wagonjwa wanaotumia
"Haya ni mafunzo muhimu Sana kwasababu tulikuwa tunajaribu kuwakumbusha wenzetu umuhimu wa kuzingatia masuala ya usalama wakati wa kufanya kazi na vyanzo vya mionzi"Alisema Salehe
Nae Mratibu wa mafunzo hayo ambae pia ni mtafiti katika Tume ya Nguvu ya Atomic Wilbroad Mlogora (TAEC ) anamsema mafunzo hayo yanalenga kuinua uelewa wa Kinga ya mionzi kwa wafanyakazi, ambao wanafanya kazi kwenye Tiba kwa njia ya X-Ray,kwani wao nitofauti na wafanyakazi wengine,kwani wao na mgonjwa wanakuwa chumba kimoja, hivyo upo uwezekano mkubwa Kama wasipopata mafunzo ya namna ya kujikinga wakapata madhara.
Kwa kwa kuzingatia hayo madhara yanaweza kuepukika ,Ila kupata mionzi hakuwezi kuepukika ,kwani inafahamika kila kitu kina madhara na faida zake,hivyo wanao uhakika kutokana na mafunzo hiyo mionzi kidogo wanayoipata, haitaweza kuwaletea madhara .
Kwa upande wa washiriki wa mafunzo hayo Idrisa Juma kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete,ambae ni Afisa mteknolojia wa Elimu ya mionzi , alisema kuwa kutokana na Elimu waliyopatiwa imezidi kuwaongezea weledi na ufanisi katika ufanyaji wa kazi, kwasababu huwa wanaendesha mitambo ya mionzi katika tiba na katika upimaji,hivyo itawasaidia kuwakinga wengine dhidi ya mionzi
Martha Emmanuel Mbona yeye ni muuguzi kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete,anasema yeye anafanya kazi katika chumba ambacho wanatumia mionzi na wanashughulika na utambuzi, uchunguzi wa mishipa ya damu ya Moyo pamoja nakuziba matundu madogo ya Moyo haswa kwa watoto na watu wazima
Hivyo Mafunzo hayo yatawasaidia katika utendaji wao wa kazi kwani yeye ni mtu wa pili kutoka kwa Daktari ,hivyo itamsaidia kujilinda na mionzi kwasababu wanapoendelea na kazi katika chumba wanakuwa pamoja na mgonjwa, hivyo Ile mionzi anayoioata mgonjwa anategemea itanipata japo kwa kiasi kidogo,kwani mafunzo aliyoyapata yatamsaidia jinsi gani itapungiza Ile dozi iwe kwenye dozi ndogo.
Mwisho
No comments