Kwa upande
wake Laigwanani mkuu Kiloriti Ole Ngulupa, alisema kuwa elimu ni bora kwa watoto wote wa kike n awa kiume kuliko kitu kingine chochote katika maisha yao,hivyo Ni kosa kisheria kumkatisha mwanafunzi masomo yake kwani unamnyima haki yake ya msingi,na ikibainika hivyo Sheria ifuate mkondo wake.
Kiloriti Alisema jamii ya wafugaji iliyopo katika wilaya ya Longido, imefanya sala kwaajili ya kuwabariki watoto
hao kwania ya kuwaombea juu ya mitihani yao wa mwisho unayofanyika tar 8-9 -2021 kwaajili ya
kuhitimu elimu yao ya darasa la saba.
‘’Hivyo kwa
sala hii tumewabariki watoto wa kila Kijiji ,tunamshukuru Munu jambo hili liwe
la wilaya nzima sisi tumeamua kuwabariki watoto weetu kwa baraka ya mila nzuri
kwasabababu tunahitaji elimu kwa watoto hawa,japokuwa matarajio ya
mzanapompeleka mtoto shule yanakuwa makubwa ,pengine pale Watoto wetu hawajasoma
kama tunatarajia
Amesema kuwa watoto wao baadhi yao wetu wanaishia darasa la saba, wengine
akifika sekondari anaanza kidato cha kwanza anaishia kidato cha pili au cha
tatu ,wanatoroka kenda nchi jirani,na wale ambao wanabahatika kwenda vyuoni
wengi wao wanakosa ajira
Akisoma risala kwa mgeni rasmi mwalimu mkuu wa shule ya Kimokouwa ,Minja alisema shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 523 ambapo wavulana 257,wasicha 266,waalimu 10 wanaume 2wanawake 8 wapishi 2 na mlinzi 1 imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma na imekuwa nafsi ya kumi bora kiwilaya.
"Hayo yanatokana nanjuhudi kubwa zinazofanywa na serikali yetu ikishirikiana na Wazazi,walezi,waalimu,pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Kimokouwa"Alisema Minja.
Aidha Minja alisema kuwa pamoja na mafanikio yote hayo ,zipo changamoto zinazo ikabili shule hiyo ikiwemo uzio eneo shule,shule kupatiwa hatimiliki tofauti na alama tu (bevons)ukarabati wa thamani na miundo mbinu chakavu,uhitaji mkubwa wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
Changamoto nyingine ni pamoja na mwamko duni wawazazi kuchangia chakula kwa wanafunzi, upungufu wa mashime ya photokopi,thamani za ofisi za waalimu pamoja na upungufu wa matundu ya vyoo vya wanafunzi na waalimu.
"Watoto hawa wakiendelezwa kielimu wanauwezo mkubwa Sana,hivyo bado mtoto wa kike anayo nafasi kubwa Sana katika jamii yetu,Unapomwelimisha mtoto wa kike unapanua wigo mkubwa kwani unaelimisha jamii nzima"Alisema Minja.
Aidha shule ya msingi Kimokouwa ulianza rasmi mwaka 1978 ikiwa na jumla ya wanafunzi 23 wavulana 13 wasichana 10 waalimu 2 na vyumba 2 vya madarasa.
Hivi Sasa shule hiyo Ina jumla ya wanafunzi 523 ambapo wavulana Ni 257 wasichana 266,waalimu 10 ,wanawake 8 wanaume 2,wapishi 2 na mlinzi 1 na vyumba vya madarasa 9
No comments