MAADHIMISHO YA MIAKA 64 YA UHURU WA TANZANIA BARA RAIS SAMIA ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 1,036
Rais Samia Suluhu Hassan leo Disemba 09, 2025, Tanzania ikiadhimisha miaka 64 ya uhuru wa Tanzania Bara ametangaza kuwasamehe wafungwa 1,036 ambapo 22 kati yao wameachiwa huru na waliobaki 1,014 wamepunguziwa adhabu.
Kulingana na taarifa iliyosainiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, Ikulu imeeleza kuwa serikali inatarajia wafungwa walioachiwa huru watarejea tena katika jamii kushirikiana na wananchi katika ujenzi wa Taifa na kujiepusha kutenda makosa.
Miongoni mwa waliosamehewa ni wafungwa wagonjwa wenye magonjwa ya kudumu au sugu ambao wapo katika hatua za mwisho pamoja na wafungwa wazee wenye umri wa miaka 70 au zaidi.
Aidha wengine walionufaika na msamaha huo ni wafungwa wa kike walioingia na ujauzito gerezani au wenye watoto wanaonyonya au wasionyonya waliohukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na kuendelea pamoja na wafungwa wenye ulemavu wa mwili na akili wasio na uwezo wa kufanya kazi.
Aidha wamesamehewa pia wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kuwekwa kizuizini ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka kumi au zaidi.
Chanzo Azam
No comments